Je, Unasoma Wapi?/Where Do You Study?

Je, Unasoma Wapi?/Where Do You Study?

Msamiati / Vocabulary

Chuo kikuu
university
darasa
class
soma
study
kozi
course
maktaba
library
Mwaka
year
kazi chache
little work
kazi nyingi
a lot of work
karatasi
paper
mshauri
advisor
Kazi ya nyumbani
homework
mwanafunzi
student
profesa
professor
kompyuta
computer
mtihani
exam
insha
essay
mwalimu
teacher
enda kwa
go by
Kalamu
pen
Gari
car
Kwenda
to go
baiskeli
bicycle
nyumbani
at home
kutembea
to walk
kupumzika
to rest
pikipiki
motor bike
kupumzika
to rest
treni
train
kuchoka
to get tired
Rahisi
easy
shahada ya kwanza
first degree
basi
bus
-gumu
hard
fanya marudio
review
wasiwasi
anxiety
uzamili
masters
utafiti
research
uzamifu
doctorate
tasnifu
thesis or dissertation
kuwasilisha
to present
mkutano
meeting
mahojiano
mahojiano
wasilisho
presentation
kongamano
conference
programu
program
mahojiano
interview
mkutano
meeting

Masomo ya Chuoni/Majors

Mazungumzo I: Neema na Erin wanakutana katika kongamano la masomo ya Kiafrika. #

Neema: Hujambo rafiki! Jina langu ni Neema.

Erin: Sijambo rafiki. Mimi ni Erin. Je, unatoka wapi Neema?

Neema: Ninatoka Dar es Salam, Tanzania. Na wewe je?

Erin: Mimi ninatoka katika mji wa Columbus, Ohio, Marekani. Je unasoma wapi?

Neema: Mimi ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Ohio State. Na wewe je?

Erin: Mimi ninasoma katika Chuo Kikuu cha Northwestern. Unasoma nini chuoni?

Neema: Ninasoma elimu ya siasa. Na wewe je, unasoma nini?

Erin: Ninasoma uandishi wa habari. Je, uko mwaka wa ngapi?

Neema: Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu. Na wewe je?

Erin: Mimi ni mwanafunzi wa uzamili. Niko katika mwaka wangu wa pili. Unapenda programu yako?

Neem: Ndiyo, ninaipenda programu yangu lakini nina kazi nyingi za nyumbani na mitihani mingi. Je, wewe unafanya mitihani?

Erin: Mimi kawaida ninaandika insha na kufanya utafiti kwa sababu ninaandika tasnifu.

Neema: Una bahati sana. Je, unaendaje chuoni?

Erin: Kawaida huenda kwa kutembea lakini mara kwa mara ninaenda kwa basi. Na wewe je?

Neema: Nilienda chuoni kwa kutembea mwaka jana kwa sababu niliishi katika bweni, lakini mwaka huu ninaenda kwa baiskeli kwa sababu ninaishi nje ya chuo. Jamani nimefurahi kukufahamu. Ningependa kuhudhuria wasilisho la mwisho.

Erin: Nimefurahi kukufahamu pia. Mimi ninasubiri mahojiano ya kazi

Neema: Kila la heri rafiki yangu.

Erin: Asante.

Zoezi I: Maswali ya Mazungumzo

i. Neema anatoka wapi?

ii. Je, Erin anatoka wapi?

iii. Je, wewe unatoka wapi?

iv. Neema anasoma katika chuo gani?

v. Erin anasoma katika chuo gani?

vi. Je, wewe unasoma katika chuo gani?

vii. Neema yuko katika mwaka gani na yuko katika programu gani?

viii. Je, wewe uko katika mwaka gani na uko katika programu gani?

ix. Erin anasoma nini chuoni?

x. Ni nani anafanya kazi za nyumbani na mitihani chuoni?

xi. Je, wewe unapenda kazi ya nyumbani au mitihani zaidi?

xii. Kwa nini Neema anafanya utafiti?

xiii. Je, wewe unafanya utafiti? Kuhusu nini?

xiv. Wewe ni mwanafunzi wa shahada gani?

xv. Je, wewe unaishi katika bweni au nje ya chuo?

xvi. Neema na Erin wanaendaje chuoni?

xvii. Je, wewe huendaje chuoni?

xviii. Je, Neema na Erin wamekutana wapi?

Zoezi II: Familia na Chuo

Je, watu katika familia yako wanasoma/walisoma katika chuo/vyuo gani?

Zoezi III: Wasilisho/Presentation

Tayarisha wasilisho fupi kuhusu maisha yako ya chuoni/Prepare a short presentation about your life at school.