Mazungumzo I #
Mgeni: Hodi! Hodi!
Mwenyeji: Karibu! (baada ya kufungua mlango). Karibu ndani.
Mgeni: Asante. Shikamoo mama. Jina langu ni Erin.
Mwenyeji: Marahaba. Hujambo? Mimi ninaitwa Mama Fatuma. Karibu kiti.
Erin: Sijambo. Asante sana, Mama Fatuma.
Mama F: Hamna shida. Habari za safari?
Erin: Nzuri sana lakini imekuwa ndefu sana.
Mama F: Pole kwa safari. Habari za familia?
Erin: Salama sana.
Mama F: Baba na mama hawajambo?
Erin: Hawajambo.
Mama F: Vizuri sana. Kaka na dada je hawajambo?
Erin: Hawajambo pia.
Mama F: Karibu Kenya.
Erin: Asante sana. Fatuma yuko wapi?
Mama F: Yeye anasoma maktabani lakini atarudi karibuni. Je, utaoga kwanza ama utakunywa chai?
Erin: Naomba kuoga kwanza.
Mama F: Sawa. Nitakuonyesha bafu ilipo.
Erin: Asante sana, mama.
Zoezi I: Mazungumzo na baba/mama wa Afrika Mashariki
With a partner, rehearse a conversation that you would have with your host mom/dad upon your arrival in East Africa.
Mazungmzo II: Fatuma na Erin #
Fatuma: Mambo Erin!
Erin: Poa. Habari gani?
Fatuma: Safi sana. Karibu Nairobi!
Erin: Asante sana dadangu. Habari za masomo?
Fatuma: Nzuri kabisa lakini nina wasiwasi wa mitihani wiki kesho. Habari za familia?
Erin: Bahati njema katika mitihani. Familia haijambo. Nimependa nyumbani kwenu sana!
Fatuma: Asante. Ungependa kufanya nini leo jioni?
Erin: Karibu dadangu. Labda nitalala mapema kwa sababu nimechoka sana.
Fatuma: Naelewa. Pole kwa safari.
Erin: Asante, lakini kesho ningependa kwenda mjini kama utakuwa na nafasi.
Fatuma: Bila shaka. Kesho sina madarasa, kwa hiyo tunaweza kwenda mjini.
Erin: Asante. Nitaenda kulala sasa.
Fatuma: Karibu na usiku mwema.
Erin: Usiku mwema pia.
Zoezi II: Mazungumzo na kaka au dada wa Afrika Mashariki
In pairs, rehearse a conversation that you might have with your host brother or sister in East Africa.