Ninapenda lakini sipendi/I Like but I Do Not Like

Ninapenda lakini sipendi/I Like but I Do Not Like

Msamiati / Vocabulary

Kuogelea
swimming
Kununua
buying
kucheza
playing
Kukwea mlima
hiking
kusafiri
traveling
kufuma
knitting
Kupika
cooking
kutembea
walking
kumtembeza mbwa
walking the dog
Kuendesha baiskeli
cycling
kukimbia
running
driving
kuendesha gari
Kucheza densi
dancing
kusoma
reading
kutazama televisheni
watching tv
fishing
Kuvua samaki
kawaida
usually
mara kwa mara
occasionally
Kwenda maktabani
going to the library
going to the movies
kenda filamuni
Kucheza michezo ya video
playing video games
kuosha vyombo
doing dishes
kusoma maktabani
reading in the library
kulima
farming or gardening
kupiga picha
taking pictures
kufanya mazoezi
working out
kucheza karata
playing cards
kuzungumza na marafiki
chatting with friends
kwenda ufukweni
going to the beach
kukutana na marafiki
meeting with friends

Mifano #

Juma: Je, kawaida wewe unapenda kufanya nini jioni?

Karim: Kawaida mimi hupenda kutazama televisheni lakini sipendi kufanya mazoezi. Kawaida mimi hufanya mazoezi asubuhi na mara kwa mara mchana. Na wewe je?

Juma: Mimi hupenda kuzungumza na marafiki wangu na kucheza michezo ya video lakini sipendi kusoma maktabani. Kawaida, sisi husoma nyumbani. Je, utafanya nini wikendi?

Karim: Wikendi nitaenda mjini kukutana na rafiki yangu. Sisi tutakula chakula mkahawani na tutaenda filamuni. Na wewe je?

Juma: Mimi nitasoma maktabani sana kwa sababu nina mtihani wiki kesho. Pia, nitaenda sokoni kununua chakula.

Karim: Utaenda sokoni pamoja na nani?

Juma: Nitaenda sokoni pamoja na mkazi mwenza wangu (roommate).

Karim: Mkazi mwenza wako anaitwa nani na anatoka wapi?

Juma: Mkazi mwenza wangu anaitwa Tim. Yeye anatoka katika mji wa Madison, jimbo la Wisconsin. Rafiki yako anaitwa nani na anatoka wapi?

Karim: Rafiki yangu anaitwa Peris. Yeye anatoka Nairobi, Kenya. Je, rafiki yako anapenda kufanya nini?

Juma: Tim anapenda kucheza michezo ya video sana na kumtembeza mbwa. Na rafiki yako je?

Karim: Peris anapenda kusafiri, kula chakula, na kutazama filamu.

Juma: Je, Peris ni mpenzi wako?

Karim: Ndiyo! Peris ni mpezi wangu. Ninampenda sana! Je, wewe una mpenzi?

Juma: Hapana, mimi sina mpenzi, lakini mkazi mwenza wangu ana mpenzi. Asante rafiki yangu. Ninakutakia wikendi njema.

Karim: Asante. Wikendi njema pia na bahati njema katika mtihani.

Juma. Asante sana.

Zoezi III: Familia inapenda kufanya nini?

Mwambie rafiki yako watu katika familia yako wanapenda kufanya nini.