Mazungumzo I: Shughuli za Asubuhi #
Rajabu: Mambo Pendo!
Pendo: Poa! Za asubuhi?
Rajabu: Freshi lakini nimechoka kidogo.
Pendo: Pole kwa kuchoka. Je, wewe hufanya nini kabla ya darasa?
Rajabu: Asante. Kawaida, mimi huamka mapema, husugua meno, hunawa uso, hufanya mazoezi ya futiboli ya Marekani, hurudi chumbani, huoga, hula chakula cha asubuhi, na huenda darasani. Na wewe je?
Pendo: Lo! Unafanya mambo mengi sana. Mimi kawaida huamka, huangalia simu, husugua meno, hunawa uso, humtembeza mbwa, husikiliza muziki, hujitayarisha, na huenda chuoni kwa basi.
Rajabu: Una bahati sana! Siku njema rafiki yangu.
Pendo: Asante. Siku njema pia.
Zoezi I: Shughuli za Asubuhi
Pamoja na rafiki, sema wewe hufanya nini asubuhi kabla ya darasa.
Zoezi II: Shughuli za Mchana, Jioni, na Usiku
With a friend, fill out the venn diagrams below with what each of you does at the different times of the day shown below and what both of you do in common in the intersection.
Shughuli za Mchana #
Shughuli za Jioni #
Shughuli za Usiku #
Note on Sarufi/Grammar #
You might have noticed that we have attached a prefix hu- to the verbs describing the activities that we perform at different times of the day. Prefix hu- indicates the habitual tense. In the next topic, we shall explore how different tenses in Swahili are marked.
Zoezi III: Scenario
Your potential host family in East Africa would like to have an idea of how your normal weekday looks like. Please use the table below to provide them with the information they have requested from you.
Saa/ Time Shughuli/ Activity Asubuhi Mchana Jioni Usiku